
Wadau wa biashara na utandawazi
Wataalam wa uchumi na biashara wanaitaja Tanzania kama moja ya mataifa yatakayonifaika zaidi na hatua yake ya kuingia katika Eneo Huru la Kibiashara Afrika yaani ‘Africa Free Trade Area' na kwamba ukuaji wa utandawazi katika biashara utaliwezesha taifa hili kumaliza umaskini kwa watu wake.
“Ni furaha kwamba Tanzania tumesaini na tunafanya taratibu za kujiunga na kinachojulikana kama eneo huru la biashara Afrika (FTA) kwasababu tumekuwa tukifanya jitihada kuimarisha biashara ya mipakani kwa kufanya tafiti na kupendekeza nini kifanywe ili tupate mapato. Sasa kama tukiingia kikamilifu katika eneo hili la kibiashara, sisis tutanufaika zaidi kama Tanzania kwasababu tunalango la kupokea na kupeleka bidhaa katika mataifa karibuni 12 amabyo hayana bandari. Na katika kitabu amabcho tumekizindua cha utandawazi na biashara, vijana wengi na wanawake wayaona namna ya kitumia utandawazi na teknolojia kukuza biashara yao katika ukanda wote wa Afrika"- Evans Exaud, Mkurugenzi Liberty Sparks.
Aidha, EA Radio imefanikiwa kuzungumza na mtaalam wa teknolojia ya habari na mawasiliano kuona nafasi ya watanzania katika kunufaika na utandawazi katika biashara, na kwamba kama vijana wa Kitanzania watakuwa tayari kutengeneza mifumo na kufanya biashara kidigitali katika kutafuta masoko na kuyahudumia basi watanufaika zaidi na fursa hii.