
Naibu Katibu Mkuu Uwekezaji, viwanda na Biashara, Ally Gugu
Hayo yanabainishwa wakati Tanzania ikiwa tayari imeanza mchakato wa kufanya biashara katika soko la pamoja Afrika chini ya mpango wa biashara huria katika eneo huru la biashara Afrika
Kwa upande wao wawakilishi wa wafanyabiashara kutoka jumuiya ya wafanyabiashara wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na sekta binafsi wameomba mpango huo kuwanufaisha zaidi wafanyabiashara kwani sekta binafsi kwani ndio inamchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi Afrika.
Kwa upande wa mwakilishi wa mwenyekiti wa Baraza la Biashara Afrika Mashariki, Raphael Maganga ambaye ni Balozi wa EABC anasema Tanzania ina uwezo mkubwa wa kuuza nje bidhaa ndani ya nchi bara la Afrika.
"Mauzo ya Tanzania barani Afrika yalifikia dola bilioni 2.5 mwaka 2021 ikiongezeka kwa asilimia 13 kutoka mwaka 2020 huku uagizaji wa bidhaa kutoka nje ukifikia dola bilioni 1.2" amesema Maganga
Naye mshauri wa sera ya uchumi kuhusu soko huru la biashara Afrika ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Lamech Wesonga, ameitaka sekta binafsi kuchukua jukumu la kufanya biashara chini ya AfCFTA ili kufungua fursa takribani bilioni 1.3 zilizopo katika soko hilo.