Jumatatu , 21st Nov , 2022

Kufuatia serikali kupitisha azma ya kuwepo kwa bima ya afya kwa kila mwananchi nchi nzima tayari sasa serikali imewataka wadau kuanzisha mafunzo kwa watoa huduma hiyo ili kuhakikisha kila mtu kwenye kila kijiji anafikiwa na huduma hiyo.

Kamishina wa Bima nchini Tanzania Dkt Bagayo Sakware

Rai hiyo imetolewa na kamishina wa bima nchini Tanzania dkt Bagayo Sakware ambaye amethibitisha kuwa soko la bima nchini bado lina uhitaji mkubwa wa wadau ambapo mara baada ya serikali kupitisha sheria za bima ya afya kwa wote uhitaji umeongezeka hivyom kuweka utaratibu sasa wa kupitia watoa huduma kuwafikia watanzania walioko vijijini

Utekelezaji wa agizo hilo umeanza ambapo kampuni ya bima ya Jubilee Alliance Insurance wameanza mchakato wa kuwaanda mawakala wa bima ambao watasambaa kila kijiji kufanya huduma hiyo wakibainisha kuwa hadi sasa ni asilimia sita tuu ya watanzxania wenye ufahamu wa bima.

Hata hivyo sekta hiyo wadau wametakiwa kuwa na maadili na kwa wale wote watakaopatiwa mafunzo watasajiliwa kama maafisa wa bima nchini wakiwa na sifa sasa ya kuwahudumia watanzania popote.