
Waziri wa Nishati January Makamba
Kauli hiyo ameitoa hii leo Mei 5, 2022, bungeni Dodoma, wakati kujadili hoja iliyotolewa na Mbunge wa Kilindi, Omari Mohamed Kigua, ya kusimamisha shughuli za Bunge zilizokuwa zikiendelea ili kujadili hali ya mfumuko wa bei ya mafuta nchini.
"Wote tunajua bei za mafuta zimepanda duniani na sisi kama nchi sio wazalishaji wa mafuta tunanunua mafuta kutoka nje na sehemu kubwa ya bei ya mafuta inayopangwa nchini inatokana na gharama ya mafuta yenyewe, gharama ya kuleta, kodi na tozo mbalimbali na gharama za kufanya biashara yenyewe hapa nchini," amesema Waziri Makamba