Ijumaa , 18th Nov , 2022

Serikali imetakiwa sasa kuzitazama upya na kuzifanyia maboresho sheria za biashara na uwekezaji kufuatia sasa kufurika kwa wawekezaji wengi kwenye sekta mbalimbali ambapo wengine wanakwama kufanya uwekezaji kulingana na kutokuwepo kwa sheria za kulinda mitaji yao endapo itatokea mkwamo.

Rais wa chama cha mawakili Tanzania TLS Prof Edward Hosea

Rai hiyo imetolewa na Rais wa chama cha mawakili Tanzania TLS Prof Edward Hosea mara katika kongamano la chama cha mawakili cha Uingereza na Tanzania ambao kwa utashi wamekubaliana kushughulikia migogoro ya kibiashara,kujadili ni sheria zipi ambazo zitakwenda kulinda mbadiliko ya tabia nchi ambayo kwa sasa ndiyo ajenda ya dunia.

Sheria nyingi za Tanzania zinatajwa kuanzia huko uingereza licha ya kuwepo kwa mabadiliko yaliyofanywa hapa nchini ambapo bado kibiashara taasisi nyingi za serikali haziingii makubaliano zenyewe kama zilivyo hivyo kuleta changamoto kubwa kwa wawekezaji wengi jambo ambali mawakili kutoka Tanzania wanaeleza umuhuimu wa wao kukutana na mawakili kutoka uingereza.

Mkutano huo unatajwa kuwa wa kipekee ukifanyika katika muda mwafaka ukitoa uhalisia wa namna uingereza wanasuluhisha matatizo ya kibiashara na sisi Tanzania ili kukuza biashara kwa pande zote.