Jumapili , 13th Nov , 2022

Serikali imewataka taasisi ya bima IIT kupitia mamlaka ya usimamizi wa bima nchini TIRA kuhakikisha inafikia asilimia 50 ya upatikanaji wa bima kwa makundi yote ifikapo mwaka 2030.

Wadau wa bima Tanzania wameadhimisha kilele cha wiki ya bima ambapo ambapo sasa inajumuisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwake ambapo pamoja na mambo mengine kizazi cha sasa kimeaswakutumia teknolojia katika kusambaza elimu ya bima kwa watanzania wote.

Hadi sasa tayari serikali imewekeza zaidi na kuagiza kuanza kwa bimaya afya kwa watanzania wote ambapo baadhi ya wataalamu na waasisi wa siku hii wamekutana kujadili namna ambavyo kila mtanzania anaweza kupata bima za majanga mbali mbali.

Hata hivyo watoa huduma wameombwa kuwa wabunifu na kuweka mifumo na huduma ambayo inaqweza kuwafikia na kutumiwa na watanzania wote katika soko la bima kwenye ujenzi wa uchumi.

Kwa upande wao washiriki wa maadhimisho hayo wamekiri kuwa kuna haja ya maksudi kuitumia teknolojia ambayo ndiyo hutumika na kizazi cha leo.