Jumanne , 29th Nov , 2022

Serikali kupitia wakala wa usambazji mbegu nchini ASA inatarajia kusambaza mbegu za alizeti za ruzuku jumla ya tani 2500 nchini nzima, ikiwa na lengo la kutoa ahueni kwa wakulima, ili kulima zao hilo kwa wingi huku wakulima wakitolewa hofu juu ya ubora wa aina ya mbegu zilizopo sasa

Katika msimu huu wa kilimo wa 2022/2023 wakulima wa zao la alizeti watanufaika kwa kupata mbegu hizo za ruzuku, ikiwa ni mkakati wa serikali katika kukuza Zaidi zao hilo la alizeti, Dkt. Sophia Kashenge mtendaji mkuu wa wakala wa mbegu nchini ASA hapa anabainisha mkakati wa serikali katika kufikia malengo

Kupitia mbegu hizo halmashauri ya Itigi mkoani Singida imepokea shehena ya mbegu hizo zitakazosambazwa kwa wakulima kama anavyosema afisa kilimo, mifugo na uvuvi wa halmashauri hiyo

Kwa upande wao wakulima wameonesha kuwa na Imani katika mpango huo wa mbegu za rukuzu katika kukabiliana na tatizo la uhaba wa Mafuta ya kula.