
Akiwa katika ziara yake wilayani Kisarawe Naibu waziri Dk. Dugange amesema kutokana na mafaniko makubwa yaliyoanza kuoneshwa na baadhi ya wajasirimali waliopatiwa mikopo serikali imeona ipo haja ya kuendelea kuwaunga mkono wajasirimali wanaoonesha muelekeo katika biashara zao.
Nae mkuu wa wilaya ya Kisarawe Nickson Simon akawataka wajasirimali wilayani humo kuhakikisha wanazalisha bidhaa zao kwa kiwango cha juu ili kuendana na soko la ushindani katika soko.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri huyo ametembelea miradi mbalimbali ikiwemo shule ya sekondari Msimu, ujenzi wa jengo la huduma za dharura hospitali ya wilaya kisarawe pamoja na ujenzi wa zahanati ya Msimbu huku akieleza kufurahishwa na kasi ya utekelezwaji wa miradi hiyo.