Alhamisi , 1st Jun , 2023

Serikali imesema imefungua milango ya majadiliano na wadau wa uwekezaji kila upande ili kuondoa changamoto tata za kikodi,kujenga miundo mbinu rafiki kusimamia sheria,sera za uwekezaji ili kuhakikisha ile nia ya utashi wa kisiasa kwenye uwekezaji inaonekana katika uhalisia kwa wawekezaji.

Hayo yanajiri mara baada kuwasilishwa kwa ripoti ya pili ya kibiashara kati ya Tanzania na nchi za scandinavia ampabo mkutano uliwakutanisha mabalozi kutoka nchi hizo na wafanyabishara baadhi ambapo akitoa taarifa ya hali ya kibiashara na utayari wa nchi kwa niaba ya waziri wa Viwanda Bishara na uwekezaji..Dr Ashatu Kijaji Mkurugenzi wa uwekezaji kutoka wizara hiyo Aristide Mbwasi amesema serikali tayari inaendelea kuboresha mazingira.

Amesema mjadala huo umelenga kutazama Kwa namna gani Tanzania inaweza kutengeneza mazingira ya uwekezaji wa muda mrefu pamoja na uwezo wa kutengeneza sera za kibiashara zenye tija ambazo zitavutia wawekezaji kutoka pembe za dunia kwenye kila sekta.

Katika mjadala huo wa wadau wa biashara,taasisi za kitafiti serikali zimejadili pia nafasi ya serikali ya Tanzania bara na visiwani kushirikina na nchi za Scandnavia ikiwemo Norway kuongeza uwekezaji wa pamoja na wafanyabiashara mmoja mmoja.

Katika upande wa utafiti imeelezwa kuwa ni vyema sasa nchi ikaanda sera maalum za uhakika zitakazoondoa upungufu uliopo wa uhitaji kwa sasa kupitia mamlaka zake za kibiashara ikiwemo kituo cha uwekezaji nchini,taasisi za usajili na utoaji wa leseni kwa wawekezaji.

Utafiti uliofanywa na taasisi ya Repoa kuhusu mazingira ya uwekezaji na ushirikiano kati ya Tanzania na nchi za Scandinavia unaonesha kwa mwaka 2022-2023 pekee makampuni yanayofanya biashara Tanzania bara na visiwani ni 99 kutoka katika nchi za Norway,Denmark,Finland,Sweden hivyo mjadala huo huenda ukaongeza tija katika uwekezaji.