Jumatano , 13th Apr , 2022

Kampuni ya bia ya Serengeti imeendeleza jitihada zake kuimarisha sekta ya kilimo nchini kwa kuongeza fursa zaidi kwa vijana wanaosoma vyuo vya ndani vya kilimo.

Hayo yamesemwa na meneja wa kiwanda cha SBL Moshi, Alice Kilembe, wakati akikabidhi vyeti vya utambulisho kwa wanufaika wa ufadhili wa masomo kwenye programu yao ijulikanayo kama Kilimo-Viwanda.

"Chuo hiki Cha Kilacha kimepata nafasi Kuwa na wanafunzi ambao tumewasaidia lengo waweze kuleta mapinduzi kwenye Kilimo katika jamii" alisema  Alice Kilembe -Meneja wa kiwanda  Cha SBL Moshi.

Wakati huo huo kampuni ya bia ya Serengeti imeendelea na programu yake ya kuisaidia jamii nchini kwa kuwakabidhi wazee wa Mwika mkoani Kilimanjaro mablanketi 150 yatakayowasaidia kwenye kipindi cha baridi kali ambapo wengi wao hupata shida na wengine kupoteza maisha.

"Hii ni eneo ambalo kama kampuni tumekuwa tukirejesha sahemu ya Faida Kwa jamii hivyo utoaji wa blanketi hizi ni ishara ya kutambua juhudi mabazo wateja wetu wamekuwa wakituunga mkono"Alice Kilembe - Meneja wa kiwanda  Cha SBL Moshi.

Mablanketi hayo yalikabidhiwa kwa niaba ya wazee kwenda kwa Mwika Rotary Club ambao pia wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha jamii ya wazee Mwika wanapata huduma bora kipindi cha uzee wao. 

"Kama kiongozi mstaafu ambaye nimekuwa hapa na kuzifahamu changamoto za wazee hawa kituoni hapa nisema Asante Kwa Kampuni ya SBL huu ni upendo wa dhati asanteni Sana."Esther Towo-rais mstaafu Mwika Rotary Club.