Jumanne , 30th Aug , 2022

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Adam Malima amesikitishwa na maandalizi mabovu ya maonesho ya biashara  ya Afrika Mashariki yanayofanyika katika uwanja wa mpira wa miguu wa Nyamagana na kuwaagiza wakuu wa wilaya ya Nyamagana na Ilemela kutafuta eneo maalum kwa ajili ya maonesho hayo

Kutokana na hali hiyo Malima ameagiza maandalizi ya kupata eneo la maonyesho yaanze sasa ili kulipa hadhi jiji la Mwanza kwa kuwa maonyesho makubwa kama haya hayawezi kufanyika uwanja wa mpira wa miguu

Akiwa kwenye maonesho hayo mwenyekiti wa taasisi ya wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo mkoa wa Mwanza Gabriel Chacha ameiomba serikali kutunga sera ya kuwafanya wafanyabishara wa sekta ya kilimo na viwanda kujiunga kwenye chemba ya wafanyabiashara

Hayo ni Maonesho ya 17 ya biashara ya Afrika Mashariki  kufanyika jijini Mwanza lengo lake likiwa ni kuendelea kuboresha wigo wa ushiriki makundi mbalimbali ya wafanyabiashara wadogo na wakubwa