Jumatano , 21st Apr , 2021

Serikali imewataka watumishi kutoka Wakala wa usajili na utoaji leseni  za biashara BRELA kuongeza kasi, kuboresha mahusiano kwa wafanyabiashara sambamba na kuweka taarifa zote sahihi endapo mtu anahitaji kufungua kampuni ama kuanzisha biashara.

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo.

Kauli hiyo imetolewa hii leo na Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo wakati alipotembelea BRELA na kuzungumza na watumishi akitoa maelekezo kuwa Kazi ya serikali ni kuwezesha  mazingira ya wawekezaji kuwekeza hivyo kuomba watumishi kutokuwa kikwazo.

Sambamba na hilo ametamani kuona watumishi waliopewa dhamana katika sekta ya biashara kuhakikisha zinatafuta masoko ya kimataifa kwa ajili ya wafanyabiashara wa ndani kuwa Dunia ya leo imejaa ushindani hivyo kuitaka pia sekta binafsi kujipanga kiushindani.

"Kazi ya serikali ni kuweka mazingira ili sekta binafsi ifanye kazi niwaombe watumishi wote kufanya kazi usiku na mchana huku wakikaa kibiashara zaidi", amesema Prof. Kitila.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa BRELA amesema kwa sasa mifumo yote iko vyema katika usajili wa makampuni kupitia mtandao.

"Kwa sasa system zetu ziko imara tofauti na huko nyuma zilikuwa na mafua mafua kidogo"Godfrey Nyaisa-Mkurugenzi mtendaji BRELA.