Awali akitoa wito katika maadhimisho hayo mjini Morogoro Waziri wa kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu prof Joyce Ndalichako amewataka waajiri kutimiza matakwa ya sheria afya na usalama mahala pa kazi katika kulinda wafanyakazi akibainisha kuwa afya ni mtaji katika taifa lolote lile.
'Ni muhimu sana waajiri wakakumbuka katika kipindi hiki ambacho nchi inavutia uwekezaji ni vyema sheria ya afya na usalama mahala pakazi ikatekelezwa'.Prof Ndalichak
Kwa upande wake mwakilishi wa shirika la kazi duniani ILO amesema ni wajibu wa nchi kutekeleza mikataba ya kimataifa iliyoingiwa inayohusu haki na madai ya wafanyakazi ili kuongeza ufanisi katika maeneo ya kazi.
Hata hivyo mtendaji mkuu kutoka OSHA Khadija Mwenda amesema kuna program mbali mbali zimeanzishwa na kuwakumbusha waajiri kuzitumia kwenye maeneo yao ya kazi ili kupata matokeo chanya kila upande akisisitiza afya na usalama kazini ni msingi imara kwa maendeleo.
'kuna program mbalimbali wakala tumeanzisha ambazo kimsingi zimelengakuleta ufanisi na usalama mahala pa kazi hivyo ni sasa waajiri wakapendezwa zaidi kutumia mifumo ya kisasa'..amesema Khadija mwenda-Mtendaji Mkuu -OSHA