Mvua Dar, mbogamboga zimesombwa na maji

Jumatano , 14th Oct , 2020

Baada ya mvua kubwa kunyesha jana Jijini Dar es Salaam, imepelekea mboga za majani kuadimika sokoni leo hali iliyopelekea fungu moja la matembele kuuzwa kati ya mia tisa hadi elfu moja na mia mbili, huku mchicha na maboga ukiuzwa shilingi 500.

Mboga za majani zikiwa Sokoni.

Wakizungumza na EATV wafanyabiashara hao wamesema kuwa kutokana na mabonde kujaa maji mboga zimeadimika leo Jijini Dar es Salaam na kwa siku ya kesho wanategemea mboga kutoka mikoa ya Morogoro na maeneo jirani.

Aidha, wafanyabisahara hao wamesema kuwa, kutokana na kukosekana huko kwa mbogamboga kumepelekea malalamiko kwa wateja kwa kuwa bei zimepanda ghafla.

"Mvua ya jana imeleta maafa mpaka kwa wafanyabiashara wa mboga za majani, mboga nyingi zinalimwa sehemu zenye mabonde hivyo zimebebwa na maji na kwa wiki hii mboga tutategemea kutoka Morogoro na maeneo jirani", amesema mmoja kati ya wafanyabiashara hao Sophia Robert.