Jumatatu , 5th Jun , 2023

Halmashauri ya jiji la Dar es salaam imetenga zaidi ya shilingi bilioni 5 kwa ajili ya kutengeneza barabara za kiwango cha lami kwenye majimbo matatu ya Ilala, Ukonga na Segerea.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji hilo Mhandisi Amani Mafuru amesema wametekeleza  agizo la serikali la kutaka Halmashauri zitenge asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya miundombinu na wamefanikiwa kwenye agizo hilo ndio maana utekelezaji umeanza mara moja.

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Halmashauri ya jiji la Dar es salaam Omary kumbilamoto amewataka wakandarasi waliopewa zabuni hiyo kufanya kazi kwa kasi ili kukamilisha mradi huo kwa wakati Pia ametoa angalizo kwa wakandarasi kutotumia vibaya mamlaka walizopewa.

Naye Mkuu wa Wilaya Ilala Edward Mpogolo  amezitaka pande zote zitakazohusika kuzingatia makubaliano yaliyo kwenye mkataba ili kusiwe na kikwazo.

Wawakilishi wa kampuni zilizopewa dhamana ya matengenezo ya barabara hizo wamesema watazingatia masharti yaliyopo kwenye mkataba na watajitoa zaidi ili kuepeuka kukwamisha mradi huo.

Wakandarasi hao wamepewa kipindi cha miezi sita kukamilisha ujenzi huo ambapo kazi ya usimamizi wa mradi huo utasimamiwa na TARURA kwa kushirikina na Halmashauri ya jiji.