Jumatano , 16th Nov , 2022

Kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu baada ya kutangazwa matokezo ya sensa ya mwaka huu Taasisi ya utafiti wa uvuvi nchini TAFIRI imeona ipo haja ya kuongeza jitihada za kupunguza upotevu wa mazao ya uvuvi ili kuongeza uzalishaji wa Samaki

Katika mafunzo maalum ambayo yameandaliwa na shirika la chakula na kilimo la umoja wa Matifa FAO ambalo limewakutanisha wadau na wataalam wa uvuvi ikiwa ni uratibu wa kubaini namna ya kupambana na tatizo hilo.lengo lake likiwa ni kupata takwimu halisi na baadae kujikita katika ufatiliaji na udhibiti wa tatizo hilo la kupunguza upotevu wa mazao ya uvuvi

‘Sasa kama walaji wa samaki wanaongezeka na kiwango cha uzalishaji kiko palepale ina maana ni lazima utafute mbadala wake na mbadala mwepesi ni kupunguza uharibifu unaotokea kwenye mazao ya uvuvi baada ya kuvua hili group litoke sasa liwe ndiyo mwenezaji wa hii Habari kwa watu wengine wengi Zaidi tukishapata jeshi la kutosha basi tuingie kutafuta takwimu za uharibifu wa mazao ya uvuvi na hatimaye tuweke mbinu na mkakati wa kushughulikia hilo tatizo’

Kwa upande wake mwakilishi wa mkurugenzi mkuu TAFIRI Hillary Mroso amesema utafiti huo utasaidia kujua hadi sasa kuna uzalishaji kiasi gani wa mazao ya uvuvi na mahitaji ni yapi

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mwanza Adam Malima, mkuu wa wilaya ya Magu Salum Kalli akatoa neno la serikali kwa kuwataka kutumia mafunzo hayo kutoa elimu Zaidi ya kudhibiti upotevu wa mazao ya uvuvi
‘Tujifunze namna ya kutunza mazalia ya samaki na namna ya kuelisha wavuvi kuvua kwenye uvuvi wa kistaarabu uvuvi unaoendana na maekezo ya mwenyekiti na wataalamu kutoka nje ya nchi ili tukuze pato la Samaki ili liyusaidie duniani’