Jumapili , 27th Nov , 2022

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Madaba kutenga maeneo ya kujenga viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya miti.

Kanali Thomas ametoa ushauri huo wakati anazungumza watendaji wa Halmashauri hiyo ambapo

Amesema hali ya hewa ya Madaba inafaa kwa mazao ya miti,parachichi na tangawizi hivyo vikianzishwa viwanda kuongeza thamani ya mazao hayo wananchi watapata faida maradufu.

Pia amewaagiza watendaji kuhakikisha mbolea ya ruzuku inawafikia wakulima jirani na maeneo wanayoishi.katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa amewaagiza watendaji katika Halmashauri ya Madaba kusimamia utekelezaji wa miradi ili iweze kukamilika ndani ya mkataba akisisitiza kuwa serikali inatoa fedha nyingi kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo