Jumatano , 20th Jul , 2022

Zaidi ya makampuni 500 kutoka ndani na nje ya nchi yanatarajiwa kushiriki  katika maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Mara International Business Expo yatakayofanyika mkoani Mara mwezi Septemba mwaka huu huku wafanya biashara zaidi ya 5000 wakitegemewa kushiriki maonyesho hayo

Mwenyekiti wa Chemba ya wafanyabiashara (TCCIA) Boniphace Ndengo

Akiongea na waandishi wa wahabri Mwenyekiti wa Chemba ya wafanyabiashara (TCCIA) Boniphace Ndengo amesema mkoa wa mara unafursa nyingi ambazo hazijafunguka hivyo kwa kuwepo kwa maonyesho haya mkoa wa mara utafunguka kibiashara na kiuchumi.

“Mkoa wetu una fursa nyingi ambazo hazijafunguka kwani Mkoa unafursa ya utalii, madini pamoja na fukwe nzuri za ziwa Victoria ambazo hazijulikani hivyo sisi kama chemba ya wafanyabiashara tumeliona hili na kuamua kuanziasha maonyesho haya ambayo yatakutanisha watu kutoka mataifa mbalimbali kutoka katika pembe zote za duania” amesema Ndengo Mmwenyekiti TCCIA.

Maonyesho ya kimataifa ya wafanyabiashara yanatarajiwa kuanza September 2 - 11 mkoani hapa katika uwanja wa kumbukumbu ya Karume ambapo katika maonyesho hayo yatajumuisha sekta zote za Madini, Kilimo, Uvuvi Viwanda pamoja na wajasiliamali wa Nyanja zote huku wafanayabiashara kutoka nje wakitegemewa kuonyesha bidhaa zao .