
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt Dorothy Gwajima, akikabidhi mtungi wa gesi kwa Mama lishe
Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt Dorothy Gwajima, ambaye pia amezitaka Halmashuri zote nchini kuja na kanzi data maalumu itakayoeleza wapi machinga walipo wangapi wamepatiwa mikopo ili kuweka dira ya kuwakuza kibiashara ndiyo azma ya kuanzishwa kwa wizara hiyo
Aidha kampuni hiyo pia imewapa mama lishe hao majiko ya gesi ya kupikia, viti vya wateja kukalia mavazi ya kuvaa wakiwa kwenye biashara zao ambapo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Unguu Sulay, akibainisha kuwa tangu serikali itenge maeneo maalum wamekuwa bega kwa bega kusaidia mama lishe na baba lishe katika wilaya mbalimbali za Dar es Salaam.
Elimu ya fedha kutunza taarifa za biashara imeonekana ni tatizo kubwa kwa kundi la mama lishe ambao wanaziomba taasisi za kifedha na wachumi kutochoka kuwapa elimu hiyo