Jumanne , 13th Sep , 2022

Tangu bei ya mafuta ilipoanza kupanda duniani, biashara ya magari na mashine zinazotumia mafuta zilitajwa kuteteleka kila kulipokucha, mambo yameonekana kuwa tofauti baada ya kushuka kwa bei ya nishati hii mhimu, wafanyabiashara wa magari wanasema biashara ya magari imeongezeka.

Wafanyabiashara wa magari

“Mafuta yalipopanda bei kwakweli ilikuwa ni changamoto kwa biashara yetu, magari yalikuwa hayauziki kwasababu watu walikuwa wanajofia bei ya mafuta. Baada ya bei mpya kutangazwa hivi majuzi tunaona kuna utofauti mkubwa sana, watu wanajiyokeza sana kununua magari, hawabaguibagui sasahivi kama ilivyokuwa zamani. Wananunuatu hata magari yenye CC kubwa watanzania wananunua sana, kwahiyo kama serikali itaendelea kuweka ruzuku tunatarajia biashara itakuwa nzuri zaidi"- Osama Samir , Mfanyabiashara wa magari Dar es Salaam. 

EATV imepata wasaa wa kuzungumza na mmoja wa raia ambaye amenunua gari Bw. Emmanuel Kombe, anasema hali ya bei ya mafuta katika soko la dunia ambayo imetangazwa kushuka imewasukuma watu wengi kununua magari wanayoyapenda bila kujali yanatumia mafuta kiasi gani.

“Kwahivi sasa kwakweli kushuka kwa bei ya mafuta kunasababisha mtu ununue gari ambalo unalitaka mwenyewe kwasababu unajua utaweza kuhimili gharama za uendeshaji wake. Mfano mimi hapa nimekuja kununua gari kwanza nimezingatia matumizi yake kwamba ninaenda kulitumia kwa majukumu gani, lakini pia nimeangalia ulaji wake wa mafuta, hii ndiyo sababu ya msingi sana"- Emmanuel Kombe, Mkazi wa Dodoma.