Alhamisi , 26th Sep , 2024

Watumiaji wa mtandao wa Airtel nchini waneshauriwa kutumia huduma ya Airtel money ili kuweza kupata nafasi ya kujipatia shilingi 20,000/=, kwa kufungua huduma ya Artel money kwa namba au Airel Money App ndani ya miezi mitatu.

Andrew Rugamba, Mkurugenzi Airtel

Mteja anaweza kupata kiasi hiki kupitia promosheni ya JIBOOST na Supa bonus, Mkurugenzi wa Airtel money Andrew Rugamba anafafanua zaidi.
“Tunafurahia kuitambulisha kampeni hii ya Jiboost na Airtel money ili kuleta thamani kwa wateja wetu, promosheni hii inetengenezwa kuwazawadia wateja wetu kila wanapotumia huduma za Airtel Money, katika maisha Yao ya kila siku kama manunuzi ya vifurushi Vya muda wa maongezi, intanet au malipo ya Serikali Kama vile luku, wateja wetu watakuwa wanufaika zaidi na kila muamala watakaofanya, tunajivunia kuwa vinara wa kutoa huduma suluhishi kupitia Airtel money kwa wateja wetu”, alisema  Andrew Rugamba, Mkurugenzi Airtel Money.

Kwa upande wake mkurugenzi wa mawasiliano Jackson Mbando anasema kampeni hiyo itadumu kwa muda wa miezi mitatu.
“Kila mteja wa Airtel atapata nafasi ya kupata kiasi hicho cha shilingi elfu20 kwenye Airtel money yake atakapofungua lakini pia tuna wateja zaidi ya milioni 19, kwahiyo kwahiyo kila mmoja atapata kiasi hicho bila kujali hali yake ya kiuchumi na itakuwa kwa wateja wa zamani na wateja wapya “, alisema Jackson Mbando, Mkurugenzi wa mawasiliano.

Nae Balozi wa Airtel, Lucas Mhuvile maarufu Kama Joti anaelezea namna ya kupata kiasi hicho.
“Ukifungua tu Aitel money yako unaikuta na hii kwa simu janja ukifungua App yako tu unaikuta na wale wa viswaswadu ukibonyeza *150*60#, unaikuta hiyo hela na ambao bado hawana linę za Airtel nawashauri wanunue ili waweze kujipatia hela hizo”, alisema Lucas Mhuvile, Balozi wa Airtel.