Jumatano , 8th Nov , 2023

Ofisi ya Hazina nchini Kenya imesema nchi hiyo inakabiliwa na uhaba wa fedha kutokana na madeni yanayoongezeka ambayo yamechelewesha utoaji wa fedha kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo. 

Fedha ya Kenya

Waziri wa Fedha nchini humo Njuguna Ndung'u, ameiambia Kamati ya Fedha na Mipango ya Taifa kuwa kuongezeka kwa madeni ya muda mfupi, kushuka kwa shilingi na viwango vya riba kubwa kumepelekea nchi hiyo kukumbwa na hali ngumu ya kifedha.

"Tuko katika hali ngumu sana ya kifedha, kwa kiasi kikubwa imeletwa na ulipaji wa madeni ya muda mfupi, viwango vya riba kubwa na shilingi inayopungua ambayo imeongeza matumizi yetu kwa Ksh145 bilioni (dola milioni 945.1)," alisema Prof Ndung'u.

Waziri wa Nishati na Petroli Davis Chirchir, amenukuliwa akisema kuwa huenda bei ya mafuta ikapanda na kufikia Ksh300 (dola 1.98) kwa lita nchini Kenya ikiwa vita kati ya Israel na Hamas vitaendelea