Jumatano , 4th Aug , 2021

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imewaagiza wafanyabishara kusitisha mara moja upandishwaji wa bei ya gesi ya kutumia majumbani na badala yake warudishe bei ya awali hadi pale itakapopokea na kupitia mapendekezo na uhalali wa wao kupandisha bei.

Mitungi ya Gesi

Taarifa hiyo imetolewa na Msemaji wa Mamlaka hiyo Titus Kaguo, wakati akizungumza kwenye kipindi cha DriveShow cha East Africa Radio.

"Gesi haishikiki na tumekuja kugundua wafanyabiashara hawa wamepandisha bei kiholela kuna utaratibu haujafuatwa na watu wameanza kulalamika, tulichofanya tumewaagiza warudishe bei walizokuwa wanatumia kabla hawajapandisha," amesema Kaguo