
Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa DSTV Ronald Baraka Shelukindo (kulia) akiwa na Yusuph Mlela wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo.
Akiongea na Waandishi wa Habari katika uzinduzi huo uliofanyika ofisi za DSTV Kinondoni Dar es salaam, Mkuu wa kitengo cha thamani kwa wateja, Hilda Nakajumo amesema,
'Mteja ukiwa na kifurushi cha Bomba ukalipia cha Family unaongezewa mpaka kifurushi cha Compact na ukiwa na Family ukalipia Compact unaongezewa Compact Plus na ukiwa Compact ukalipia Compact Plus unapelekwa kifurushi cha Premium ambapo utaweza kuweza kushuhudia michezo yote duninia na burudani nyingine nyingi zikiwemo tamthilia'.
Mapema leo wakati wa uzinduzi wa kampeni ambapo yalifanyika matembezi
Naye Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa DSTV Ronald Baraka Shelukindo, amesema huu ni mwendelezo wa ofa zao mbalimbali, huku akiwataka watu kuchangamkia fursa hiyo ndani ya mwezi Machi.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa @dstvtz @Barakashelu1 akiongea kwenye uzinduzi wa ofa mpya ya #JiongezeTukuongezee ambapo wateja wa #DSTV wataweza kujipatia vifurushi vya juu zaidi wakilipia cha juu ya kile alichonacho, kama anavyoeleza hapo. pic.twitter.com/loLWMlzvMc
— East Africa TV (@eastafricatv) March 3, 2020
Kwa upande wake Balozi wa DSTV muigizaji Yusuph Mlela amesema ubora wa ofa hiyo unawagusa moja kwa moja mashabiki zake na watanufaika na kuweza kutazama tamthlia aliyoshiriki ya Sarafu ambayo inarushwa kupitia chaneli ya Maisha Magic Bongo.
Tazama Video zaidi hapa chini