
Mkuu wa wilaya ya Ilala Ng'wilabuzu Ludigija.
Mkuu wa wilaya ya Ilala Ludigija katika ziara ya kukagua miradi amesema kumekuwa na ujanja ujanja wa baadhi ya wakandarasi kufanya udanganyifu wakati wa kuagiza vifaa vya Ujenzi ikiwemo mchanga na kokoto hivyo kukwamisha Kasi ya Ujenzi wa miradi Kwa wakati na kuisababiashia serikali harasa ya kujenga mara mbilimbili
"Sasa tumeamua kupitia kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Ilala tutahakikisha tunafuatilia Kwa karibu miradi yote inayotekelezwa ili ijengwe Kwa ubora kama mikataba inavyoelekeza" amese Ng'wilabuzu Ludigija-Mkuu wa wilaya ya Ilala
Ziara ya Kamati yavukinzi na usalama imefanyika Kwa siku mbili ambaoo imekagua Ujenzi wa vituo vya afya ambayo vinajengwa Kwa fedha za tozo,Ujenzi na upanuzi wa soko la kigogo fresh ambalo kinajengwa wa fedha za uviko sambamba na Ujenzi wa shule ya sekondari Liwiti ambayo inajemgwa Kwa mtindo wa ghorofa na mradi wake utagharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.4