Jumanne , 20th Sep , 2022

Benki ya CRDB imesema vyombo vya habari vimekuwa na mchango mkubwa uliofanikisha benki hiyo kutambulika kimataifa na kupata tuzo mbalimbali zilizotokana na utoaji wa huduma bora kwenye jamii

Mkurugenzi wa Mawasiliano na mahusiano wa benki ya CRDB Tuliesta Mwambapa

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa CRDB Benki Media Day 2022 iliyowakutanisha wakuu wa vyombo vya habari pamoja na wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Mawasiliano na mahusiano wa Benki hiyo Tuliesta Mwambapa amesema vyombo vya habari kama vitashirikishwa katika nyanja ya kukuza uchumi vitasaidia kuwa na uelewa mpana zaidi wa kutanbua jukumu lao katika kukuza uchumi katika nchi yao

Akitoa mada Juu ya ripoti ya hesabu za fedha zinavyiwasilishwa  kwenye vyombo vya habari Samweli Karoli kutoka price water copers ameshauri kuwepo na uelewa ambao itansaidia mwasilishaji kutanbua kama anachokiwasilisha kwenye jamii kitaweza kumsaidia Mtanzania wa Hali ya chini sambamba na kufanya tafiti zaidi kabla ya kukiwasilisha
Nao washiriki wa CRDB Benki Media Day 2022 wameeleza namna walivyonufaika na mkutano huo na kueleza kwamba Elimu waliyoipata imekuwa na nuelekeo mzuri kwenye kuandika habari za uchumi