Jumamosi , 20th Aug , 2022

Katibu wa  Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shaka Hamdu Shaka amemuagiza Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kumuondoa haraka Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Tabora kwa kukwamisha jitihada zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan za kuwainua wakulima wa zao la Tumbaku 

Shaka ametoa maagizo hayo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ufumula wilayani Uyui mkoani Tabora ambapo akiwa hapo alipokea malalamiko  mbalimbali ya  wakulima wa zao tumbaku na miongoni mwa malalamiko ni ya kuwepo kwa urasimu wa kusajiliwa vyama vya msingi(AMCOS).

Akizungumza wakati anatoa maagizo hayo Shaka amesema amepokea malalamiko ya Mrajisi wa vyama vya ushirika mkoa wa Tabora Geophrey Chiliga kuwa na changamoto mbalimbali zinazokwamisha jitihada za wakulima. 

 “Changamoto za bwana huyu imekuwa donda sugu , tumetoka Kaliua analalamikiiwa, tumetoka Sikonge analalamikiwa, tumetoka Urambo analalamikiwa, leo tuko Uyui watu wanalia na huyu bwana. Urasimu umekuwa mkubwa sana.