Alhamisi , 2nd Aug , 2018

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesimamisha shughuli zote za Bank M na kuiweka chini ya uangalizi wake kuanzia leo hii Agosti 2, 2018.

Nembo ya Bank M pamoja na Benki kuu ya Tanzania 'BoT' (kulia)

Benki Kuu imechukua uamuzi huo baada ya kubaini Bank M inaupungufu mkubwa wa ukwasi kinyume na sheria ya mabenki na taasisi za kifedha ya mwaka 2006.

Hayo yamebainishwa na Gavana wa benki Kuu ya Tanzania, Profesa Florens Luoga wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, na kusema kabla ya kuchukua maamuzi hayo benki hiyo iliongozewa muda wa mwezi mmoja ili iweze kukamilisha taratibu za mtaji lakini kwa bahati mbaya wameshindwa kufanya hivyo.

Ikumbukwe Januari 4, 2018 BoT ilizipa miezi sita benki tatu ili ziweze kuongeza kiwango cha mtaji unaohitajika kutokana na matakwa ya kisheria ya kuwa na mtaji kamili wa kutosha.

Benki hizo ni Kilimanjaro Co-Operative Bank Limited, Tanzania Women Bank Plc na Tandahima Community Bank Limited ambapo zilipaswa zitekeleze hayo kabla Juni 30, 2018

 Kwa taarifa kamili soma hapa