
Wafanyabiashara hao wametoa kauli hiyo wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Tanga Rajab Abdulrahman baada ya kutembelea wafanyabiashara hao na kufahamu hali halisi ya bei za bidhaa za vyakula katika masoko yaliyopo katika jiji la Tanga.
Aidha, Mwenyekiti wa CCM Mkoa Tanga amesema ziara hiyo inalenga kusikiliza kero kutoka kwa wafanyabiashara na wateja wao na kuzitafutia ufumbuzi ikiwa ni agizo Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.