Alhamisi , 15th Sep , 2022

Ili Kuboresha huduma za kifedha kwa watanzania, BancABC tayari imezindua utaratibu wa riba kwa wateja watakaofungua  akaunti za amana amabapo watapata riba ya hadi asilimia 11 papo hapo baada tu ya kujiunga na benki hiyo. 

Bi. Joyce Malai, Afisa mkuu muendeshaji BancABC Tanzania

Akizungumzia kampeni hiyo Mara baada ya uzinduzi Afisa mkuu muendeshaji BancABC Tanzania, Bi.  Joyce Malai amesema kampeni hiyo itadumu Kwa takribani Miezi mitatu kuanzia Septemba 15 huku  akiwataka Watanzania sasa kufaidika na huduma hiyo. 

Hata hivyo meneja kitengo Cha wateja wa rejareja na biashara Lilian Mwakitalima amesema wamejidhatiti na kwamba pale mteja atakapo fungua tuu atapatiwa riba hiyo akiwasihi kutembelea katika tawi lolote Ili kufungua akaunti ya Amana ambayo inaweza kumsaidia pia kupata mkopo.