Jumatatu , 10th Apr , 2023

Benki ya BancABC Tanzania, imesema itaendelea kuwekeza kwenye bidhaa na huduma bunifu ili kuendana na hali halisi ya maisha ya kila ya wateja wake.

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC Tanzania Imani John wakati wa futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake.

‘Tumeandaa futari hii ili kuonyesha Umoja na vile tunavyowajali wateja wetu’, alisema Iman huku akisema kuwa benki hiyo imekuwa na utamanduni wa muda mrefu wa kuandaa futari ikiwa ni ishara ya kuonyesha upendo kwa kipindi cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Katika futari hiyo iliyowakutanisha zaidi watu ya 300 wakiongozwa na Kaimu Shehe Mkuu Mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Walid Al-hadi Omar ambaye amewataka Watanzania bila ya kujali dini zao kuonyesha Umoja na mshikamano wakati huu wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Ni kawaida kwa mashirika ya kifedha kuwekeza sehemu ambayo wana uhakika wa kurundisha faida. Lakini BancABC imeonyesha utofauti kwani imeenda hatua mbele na kwa kweli huu ni mfano wa kupongezwa’, alisema Omar huku pia akiipongeza benki hiyo kwa kuendelea kuunga mkono miradi ya maendeleo na hasa kwa Mkoa wa Dar es Salaam.

Imani aliongeza kuwa BancABC imejikita kwenye huduma za kimtandao “kidijitali” ili kuwezesha Watanzania wengi walio nje na ndani ya nchi kuendelea kufanya miamala na kukuza pato la Taifa.