
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba
Kauli hiyo imetolewa hii leo Septemba 14, 2022, na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba, katika mkutano ulioandaliwa na Benki ya Dunia kupitia MIGA kitengo ambacho kinawahakikishia wawekezaji kuwekeza nchi mbalimbali za Afrika ambapo Tanzania imetajwa kama nchi ambayo kwa sasa imejipambanua katika kufungua milango yake Kwa ajili ya wawekezaji kuingiza mitaji yao kwenye sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo na utalii.
Mkutano huo umewahakikishia wawekezaji kutumia fursa zilizofunguliwa na serikali kufika kutengeneza fursa za ajira na kuongeza kipato.