Amezaliwa Agosti 19, Mtanzania aliyekulia nchini Sweden. Amepata elimu yake katika vyuo vya Fryshusets gymnasium huko Stockholm, Sweden, Fryshusets KunskapsCentrum na Jämtlands Län, Sweden.Ameshawahi kuwa mtayarishaji wa vipindi na mtangazaji wa kipindi maarufu ‘Nirvana’ cha EATV na ni mkufunzi wa kucheza muziki aliyetunikiwa cheti cha mafunzo ya miaka mitatu huko Stocklohom - Sweden. Amebobea katika mafunzo ya kucheza muziki wa kisasa aina ya Hip Hop, Jazz, Ballet na Contemporary dance.