PRESENTERS

TONY ALBERT
+
TONY ALBERT

Amezaliwa Tarehe 10/06 Mwanza na kukulia ndani ya jiji la Dar es Salaam.Amesoma shule za Esaacs Primary School na Kampala International High School.
Tbway ana urefu wa futi 6.5 . Anapenda sana kupiga picha, kuogelea, movie na kuendesha magari kwa kasi. Alipachikwa jina la TBWAY 360 akiwa na umri wa miaka 14 baada ya kuzungusha gari mzunguko wa duara yaani nyuzi 360

MAGGIE VAMPIRE
+
MAGGIE VAMPIRE

Nimeshiriki miss universe mwaka 2011 mara baada ya kumaliza chuo  na kufanikiwa kuingia katika Top finalist.

Vilevile mwaka uliyofuata nilishiriki  miss Tanzania na kufanikiwa kushinda taji dogo la top Model (fast track)

na pia kufika hatua za juu za miss Tanzania top 5 finalist 2012.

Napendelea kufanya mazoezi, kuogelea, kucheza mziki, kusafiri, kukutana na marafiki wapya ili kubadilishana mawazo,

Napendelea pia kuangalia Cinema mbali mbali na kujifunza vitu vipya.

Sponsored BY

JUDGES

SHETTA
+

Shetta alizaliwa mnamo mwaka 1990, alianza kazi ya burudani mnamo mwaka 2001 kama dancer kwenye kikundi cha Misifa camp crew kiliichokua kinamilikiwa na mwanamziki Dully Sykes. Alianza kurekodi mziki mwaka 2004 akiwa shule ya Msingi chini ya lebo ya mziki Dhahabu Records. Alipata mafanikio makubwa mwaka 2009 katika nyimbo Na play aliyomshirikisha mwanamziki Mwana FA ( Hamisi Mwinjuma). Hivi sasa Shetta anashiriki katika matamasha mbalimbali kama Kili, Sauti za Busara pamoja na matamasha nje ya nchi kama Norway, Burundi, Kenya, Uganda, Ubelgiji na uitaliano. Katika mafanikio aliyonayo Shetta ni pamoja na nyimbo zake kuonyeshwa na television za kimataifa kama Trace Urban, Chanel O na MTV Base. Licha ya  kuimba Shetta ni mchezaji mzuri wa mziki hasa miondoko ya Dansi ambayo inavyoneshwa kwenye miziki yake ya dansi kama Shikorobo.

Queen Darleen
+

Queen Darleen kama anavyojulikana na wengi amezaliwa tarehe 4 Novemba. Ni mwanamuziki mkongwe wa kike anayeimba muziki wa kufoka maarufu kama ‘rap’. Alianza kujihusisha na muziki mapema wakati muziki wa bongo fleva unaanza kushika chati hapa nchini. Amekuwa mwanamuziki kinara wa kike aliyedhamiria kuleta utofauti katika tasnia ya muziki hasa wa kufoka ambao ulitawaliwa zaidi na wanamuziki wa kiume. Mpaka kufikia mwanzoni mwa miaka ya 2000 Queen Darleen alishajiweka katika ramani na kutambulika kati ya wanamuziki wa muziki wa bongo flava nchini na mnamo mwaka 2012 hilo lilidhihirika  alipopata tuzo ya Kilimanjaro kwa nyimbo yake ya 'Maneno Maneno' aliyomshirikisha mkongwe wa muziki Dully Sykes, kama wimbo bora wa Dancehall mwaka. Mpaka sasa ameshatoa albam 1 na nyimbo tatu zilizoko kwenye chati mbalimbali nchini. Kwa sasa anafanya kazi na wanamuziki wakubwa akiwemo Diamond Platnumz. Licha ya ku-rap, pia anaimba na anacheza. Katika muda wake wa ziada moja ya vitu anavyofanya ni kufundisha vijana wadogo miondoko mbalimbali ya ku-dance

Super Nyamwela
+

Alizaliwa mnamo mwaka 1977 katika mkoa wa Ruvuma wilaya ya Tunduru. Alisoma na kumalizia elimu yake ya msingi akiwa huko. Rasmi alijiingiza katika fani ya muziki mwanzoni mwa miaka ya 1990 akiwa kama mcheza show katika kumbi mbali mbali za burudani huko na baadae kuhamia katika jiji la Dar-es-salaam huku akiendeleza kipaji alichokua nacho cha kucheza miziki tofauti tofauti kipindi hicho ikijulikana kama breakdance.

Ni kiongozi wa wacheza shoo katika bendi ya Extra Bongo na ni miongoni mwa wanenguaji mahiri na waliodumu katika fani hiyo kwa miaka mingi ambapo amekua mkufunzi na kiongozi wa wachezaji katika bendi ya Twanga Pepeta kwa miaka zaidi ya 10. Nyamwela amefungua chuo cha sanaa kinachofundisha taaluma mbalimbali zinazohusiana na ngoma na nyimbo za asili, ili kukuza utamaduni wa Tanzania. 

ARTICLES

"Ubunifu katika mashindano", moja kati ya makundi yaliyojitokeza 'The Quest Crew' wakiwa wamevaa kininja.

8 Aug . 2015

Makundi yaliyofanikiwa kuingia robo fainali kutokea hapa Don Bosco Upanga katika mashindano ya #2015Dance100

1 Aug . 2015

Moja ya makundi, Mavuno Crew wakionyesha uwezo wao mbele ya majaji katika michuano ya usahili wa pili leo

1 Aug . 2015

usahili wa kwanza Dance100%2015 uliofanyika TMK jijini Dar es Salaam

26 Jul . 2015

Dance 100%

4 Jul . 2015

Pages

Dance 100% ni shindano la nguvu kinoma ambalo huandaliwa na kituo cha television cha EATV na hufanyika kila mwaka kwa muda maalum uliopangwa.

Shindano hili lipo kimtaani zaidi, maana hutembelea mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam na kuweka vituo vyake kwaajili ya kufanya usajili wa makundi ya wachezaji (dancers) ambao wanapenda kucheza, kisha baada ya hapo hufanya mchujo katika vituo hivyo na kuchukua makundi matano ya washindi toka katika kila kituo na kuwapambanisha pamoja.

Lengo kuu la shindano hili ni kuwakutanisha vijana mbalimbali wenye uwezo wa kucheza ,na kisha kuwafanya wajulikane na watu tofauti kupitia kipindi hiki.

Washindi wanaopatikana katika shindano hili huzawadiwa fedha taslimu na zawadi nyinginezo kama zipo, kwa kuwapa zawadi washindi hawa huwafanya waweze kununua vifaa mbalimbali wanavyoviitaji katika sanaa yao na pia kuweza kufanya mambo yao mengine tofauti.

Washiriki katika shindano hili hucheza nyimbo mbalimbali zikiwemo reggae, R&B, Hip Hop na nyinginezo, na pia ili mtu aweze kushiriki anapaswa awe na kikundi cha wenzake kuanzia watu 5 hadi 8, mwenye afya njema, umri wa kuanzia miaka 18 (kama ana chini ya miaka hiyo anapaswa aje ana kibali toka kwa wazazi)