Jumamosi , 25th Oct , 2014

Staa wa muziki kutoka Nigeria, Ayodeji Ibrahim Balogun maarufu zaidi kama Wizkid, amekamilisha kazi ya upigaji picha za video ya Don't Cry na wasanii Radio pamoja na Weasel huko Uganda.

Weasel, Wizkid, Radio

Wizkid anayefanya vizuri katika anga za kimataifa, akifanikiwa kuwaweka katika rekodi zake wasanii wakubwa akiwepo Tyga, Chris Brown na wengine, sambamba na upigaji picha za video hii, pia ameweza kutumbuiza huko Uganda na vilevile Kenya katika ziara yake hii kubwa Afrika Mashariki.

Matunda yanayotokana na ziara ya staa huyu pia ni pamoja na kolabo na msanii Victoria Kimani ambaye walikutana na huko Kenya na kupata nafasi ya kufanya kazi studio kwa pamoja.