Ijumaa , 30th Mei , 2014

Polisi nchini Uganda wanafanya uchunguzi dhidi ya mwanamuziki Moses Sekibogo maarufu kama Mowzey Radio wa kundi la Goodlyfe kwa tuhuma za kuharibu mali kwa makusudi, kushambulia na kuwa na bangi.

Kwa mujibu wa rekodi za polisi, Radio alihusika katika ugomvi wa kutwangana ngumi na Jeff Kiwanuka, ambaye ni meneja wa zamani wa kundi hilo.

Mwanamuziki huyo anadaiwa kuvunja kiio cha gari la Kiwanuka katika baa ya Casablanca iliyopo eneo la Kololo, siku ya jumapili, taarifa za polisi zimeeleza.

Baada ya tukio hilo Radio alikamatwa na polisi nyumbani kwake huko Kizungu, tarafa ya Makidye siku ya Jumatatu asubuhi baada ya kuwakwepa polisi ambapo pia walikuta mimea ya bangi iliyopandwa na kuing'oa.