Jumatatu , 28th Apr , 2014

Kundi la muziki la Goodlyfe la nchini Uganda, linaloundwa na Mose Radio pamoja na Weasel TV, limeweza kujijengea heshima nyingine kubwa kutoka katika sherehe za ugawaji tuzo za muziki za Zzina huko Uganda, ambapo wasanii hawa wamepata tuzo 5.

Vipengele ambavyo vimeweza kuling'arisha tuzo hizi ni kile cha kolabo bora, na kolabo bora inayohusisha msanii kutoka nje ya bara la Afrika, ngoma kali ya mwaka, na hii ni kupitia ngoma yao ya Amaaso waliyofanya na msanii Pallaso, vilevile tuzo nyingine zikitoka katika kipengele cha kundi bora la mwaka pamoja na wimbo bora wa mapenzi.

Wasanii wengine walioibuka na tuzo katika sherehe hizi ni Bebe Cool kama mkali wa kumiliki jukwaa, Rema Namakula kama msanii bora wa kike kati ya mastaa wengine wakubwa.