Ruksa kuikosoa serikali - Hassan Abbasi

Monday , 19th Jun , 2017

Mkurugenzi wa Habari Maelezo Dkt. Hassan Abbasi amefunguka na kusema hakuna chombo cha habari ambacho kitachukuliwa hatua na serikali kwa kuandika habari zenye mrengo wa kukosoa sera na utekelezaji wake na kusema watu wamekuwa wakipotosha umma.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Hassan Abbasi.

Dkt. Abbasi amesema kuwa Sheria na 12 ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 kifungu cha 51 kinatoa ruhusa kwa chombo cha habari kukosoa kwa lengo la kuonyesha njia mbadala katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.

“Hakuna chombo cha habari kitakachochukuliwa hatua kwa kukosoa, haki hiyo ipo kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 kifungu cha 51, tutaendelea kuthamini na kufanyia kazi ukosoaji huo,” alisema Dkt. Abbasi.

Mbali na hilo Dkt. Hassan Abbasi amedai kuwa kama serikali haitasita kuvichukulia hatua vyombo vya habari vyote ambavyo vitakiuka sheria na misingi ya maadili ya taaluma ya habari kwa lengo la kulinda maslahi ya taifa. 

Dkt. Abbasi alisitiza kuwa ni vyema wamiliki wa vyombo vya habari wakatumia uhuru huo wa kisheria kuchapisha habari zenye nia njema kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi badala ya kueneza hofu miongoni ya mwa jamii.

Recent Posts

Mkongwe TID

Entertainment
TID ataka wakongwe wathaminiwe

Riyama Ally akiwa na mumewe Haji Mwalimu Mzee 'Leo Mysterio'.

Entertainment
Niachieni mume wangu, sie twazidi kupendana!

Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro

Current Affairs
Sirro aahidi amani siku ya Eid

Msanii wa Bongo fleva, Foby

Entertainment
Foby amtamani Ben Pol
Entertainment
Nay akomaa na Msodoki