Jumatano , 17th Apr , 2024

Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Mikiness Chisunga (39) amepoteza kichanga wake baada ya kujifungulia nyumbani kutokana na Zahanati ya kijiji cha  Namwangwa wilayani Mbozi mkoani Songwe kukosa muhudumu wa afya.

Mikiness Chisunga akiwa kwenye maumivu makali baada ya kufiwa na kichanga wake

Akiwa nyumbani kwake mwanamke huyo ameshindwa kuelezea tukio hilo baada kudai anakabiliwa na maumivu makali yanayotokana na kukosa huduma yoyote ya kimatibabu

Baba wa familia hiyo Bw. Enock Kaminyoge amesema kuwa  tukio hilo limetokea wakati akifanya jitihada za  kumpeleka mke wake katika Zahanati ya  kijiji jirani.

Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw. Shida Mwampashi amesema kuwa wananchi wanaokadiriwa kufikia 800 wakiwemo wa  vijiji jirani wanakosa huduma za afya kwa sasa kutokana na Zahanati kufungwa kwa kukosa muhudumu.

EATV inaendelea kufanya jitihada za kumtafuta Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mbozi ili kuelezea utatuzi wa changamoto hiyo.