Ripoti
Timu ya mpira wa kikapu ya jiji la Cairo(Misri) yashinda ubingwa wa MAJIJI kanda ya tano baada ya kuwafunga Garowe City(Puntland-Somalia) kwa vikapu 88-74.
Timu ya taifa ya vijana wa chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes, imejiweka katika wakati mgumu kufuzu kwa mataifa ya Afrika mwakani nchini Senegal baada ya kufungwa 2-0 na Flying Eagles wa Nigeria.
Mtanzania anayecheza mchezo wa Yoga nchini Ujerumani, Michael Yoga, amesema Wizara za michezo na Ardhi zimekwamisha mpango wake wa kujenga chuo kitakachowasaidia vijana wa kitanzania wenye vipaji mbali mbali vya michezo.