Mabalozi kufanya ziara ya utalii Tanzania
Katika kuendelea kukuza Diplomasia ya Uchumi, Tanzania inatarajia kufanya ziara ya Wanadiplomasia wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania pamoja na mashirika ya kimataifa kwa lengo la kuitangaza Tanzania kama kituo bora cha utalii na uwekezaji.