Kenzo akosa matumaini
Msanii wa muziki wa nchini Kenya, Kenzo amesema kuwa, matumaini ya uhai wa muziki wake katika siku za mbeleni yapo katika giza nene, na hii ni baada ya hatua ya lebo ya Ogopa Deejayz kusitisha mikataba waliyokuwa nayo na wasanii wake hivi karibuni.