Sunday , 20th Apr , 2014

Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Salum Mayanga ametangaza wachezaji wengine 23 watakaoingia kambini April 20 kuungana na 16 waliotajwa awali kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi itakayochezwa April 26 mwaka huu jijini Dar es salaam

Wachezaji wa Taifa Stars wakishangilia goli katika moja ya mechi walizocheza katika uwanja wa Taifa,DSM

Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Salum Mayanga ametangaza wachezaji wengine 23 watakaoingia kambini April 20 kuungana na 16 waliotajwa awali katika mpango wa maboresho ya timu hiyo kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi itakayochezwa Aprili 26 mwaka huu.

Akitangaza kikosi hicho, Mayanga amesema miongoni mwa wachezaji hao 23,wachezaji 8 wanatoka Azam ,5 Yanga wachezaji ,Simba Wachezaji 4 pamoja na Hassani Mwasikili aliyeitwa kwanza ya kwanza kutoka Mbeya City ambapo wachezaji wa wanaocheza TP Mazembe Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu pamoja na Mwinyi kazimoto kutoka Quarter wakiitwa katika kikosi hicho

Katika kikosi hicho,Kocha Mayanga amewatema wachezaji Ivo Mapunda anayechezea katika klabu ya Simba na Nurdin Haroub Kanavaro anayekipiga katika klabu ya soka ya Dar es salaam Young Africans Maarufu kama Yanga.