Vijiji Mkoa Tanga vyaathirika na mvua za masika
Wakazi wa vijiji sita wilayani Kilindi mkoani Tanga nchini Tanzania wameathirika na mvua za masika zinazoendelea kunyesha kufuatia kingo za bwawa kubwa mkoani humo kusombwa na maji na kusababisha mafuriko katika baadhi ya vijiji hivyo.