Wizara yatoa maagizo kuhusu walimu wapya
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi nchini Tanzania imewataka maofisa wa elimu wa mikoa na wilaya kuwapoka na kuwaelekeza walimu wapya wanaoripoti katika vituo vyao vya kazi, hali itakayosaidia waalimu hao kudumu katika shule wanazopangiwa.