Wizara yatangaza mikakati kwa waathirika wa UKIMWI
Serikali ya Tanzania imesema imeweka mikakati mbalimbali ya kuwahudumia watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi ikiwa ni pamoja na kutoa huduma za tiba na matunzo pamoja na kuwaanzishia wagonjwa wapya dawa za kupunguza makali ya virus vya Ukimwi ARV.

