Jengeni katika halmashauri mpya kwanza - Serikali
Serikali imeliomba shirika la nyumba la taifa NHC kuelekeza nguvu zake kujenga nyumba kwenye halmashauri mpya kabla ya zile za zamani, ili kukabiliana na ukosefu wa makazi kwa watumishi wanaofanya kazi katika halmashauri hizo.

