NBA kuzindua ligi ya mpira wa kikapu kwa vijana
Shirikisho la Mpira wa Kikapu NBA litazindua rasmi msimu wa kwanza wa ligi ya mpira wa kikapu kwa vijana kwenye kituo cha vijana cha Michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete jijini Dar es Salaam mnamo tarehe 27 Februari mwaka huu.

