Tume ya kurejesha wakimbizi Burundi kuanza kazi
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR nchini Burundi linasema suala la urejeshwaji wa hiari kwa wakimbizi wa nchi hiyo linatarajiwa kupatiwa msukumo baada ya kuundwa kwa tume mpya itakayoratibu mchakato huo.