Polisi waliowafanyia ukatili wanafunzi wafukuzwa
Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya limewafukuza kazi askari wake wawili kutokana na kuwafanyia vitendo vinavyokwenda kinyume cha maadili wanafunzi wa kike wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Isuto Kata ya Isuto, Wilaya ya Kipolisi Mbalizi.